Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, matembezi hayo ya kipekee yaliandaliwa kwa juhudi za Jumuiya ya Baqi‘ ya Chicago, yalifanyika katika jiji la Mumbai, India, ambapo wafuasi wa madhehebu mbalimbali walikusanyika na kupaza sauti ya pamoja kupinga uharibifu wa Baqi‘ na kuhimiza ujenzi upya wa makaburi matukufu ya kizazi cha Mtume (s.a.w).
Ushiriki wa Wawakilishi wa Dini Mbalimbali: Umoja kwa Ajili ya kuwahami Ahlul Bayt (a.s)
Marasim hii iliyofana ilihudhuriwa na viongozi wa kidini na kijamii kutoka dini tofauti, ka vile; dini ya wahindu, waislamu, Sikh na wakristo. Kwa sauti ya pamoja, waliukosoa uharibifu wa makaburi hayo kama kitendo cha uhalifu mkubwa, huku wakitaka makaburi hayo matukufu yahuishwe tena.
Hotuba za wanazuoni na viongozi wa kidini
Hujjatul Islam Aslam Rizvi, katika mazungumzo yake alisisitiza: "Hatutakaa kwa utulivu majumbani mwetu hadi makaburi ya wana wa Mtume (s.a.w) katika Baqi‘ yatakapo karabatiwa.
Hujjatul Islam Asghar Haidari naye alikemea kimya cha baadhi ya watu kwa kusema: "Wale wanaopiga kelele kwa ajili ya kaburi la Aurangzeb, kwa nini wananyamaza kuhusu makaburi ya wana wa Mtume?"
Mshikamano wa dini nyingine kwa lengo la kibinadamu na kimaadili
Kiongozi wa Kihindu, Dkt. Swami Vishwas Nanda, alisema:
"Nitakwenda Saudi Arabia pamoja na Hujjatul Islam Rizvi na kushiriki juhudi za ujenzi wa makaburi ya Baqi‘. Sisi Wahindu pia tutachangia kifedha katika jukumu hili."
Ahuja, kiongozi wa jamii ya Sikh, aliwaambia watu wa India: "Upinzani huu utazaa matunda."
Badi‘uz-Zaman, mwanaharakati wa Kisunni, alimtaka Mfalme wa Saudi Arabia kuunga mkono ombi hili la haki na kuongeza kuwa: "Hili ni suala linalowahusu mabinti wa Mtume, Ahlul Bayt, Maswahaba na wake zake Mtume."
Washairi kwa ajili ya Baqi‘: Walisoma mashairi yao kwa Hisia huku wakipaza sauti.
Kabla ya kuanza kwa maandamano, kulifanyika tukio la kiutamaduni la mashairi ya pamoja (mushaira), ambapo washairi walisoma mashairi kwa hisia za kina, huku wakidhihirisha dhuluma dhidi ya Baqi‘ na kuonyesha upendo wao kwa Ahlul Bayt kupitia mashairi ya kusisimua.
Maoni yako